Jaji mkuu wa Kenya
Willy Mutunga,ametangaza kuwa anatishwa na baadhi ya wanasiasa na mkuu wa
utumishi wa umma vitisho ambavyo anavitasfiri kama njama ya kumshinikizwa
kutekeleza maslahi yao.
Madai haya yanajiri
wakati Kenya ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika chini ya wiki
mbili.
Jaji Mutunga ameelezea
kuwa alipokea vitisho hivi karibuni wakati kesi iliyowahusisha mgombea wa urais
Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto ilipokuwa inasikilizwa.
Wawili hao ni washukiwa
wa uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC na mahakama kuu ya Kenya wiki jana
ilipaswa kuamua ikiwa washukiwa hao wanaweza kugombea urais au la.
Uamuzi uliotolewa na
mahakama hiyo hata hivyo ulisema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuamua kesi
hiyo na kwamba mahakama ya juu zaidi Kenya ndiyo ina uwezo pekee kutoa uamuzi.
Jaji mkuu Willy Mutunga
alisema kuwa ujumbe wa barua aliyopkea ulikuwa unamtisha kuwa angetendewa jambo
baya na kundi haramu la Mungiki.
Kundi hilo pia
lilihusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007 ambapo ilisemekana
kuwa Uhuru Kenyatta alidaiwa kulitumia kushambulia watu wa kabila la Kalenjin
mkoani Rift Valley.
Mutunga aliituhumu
serikali kwa kumfanyia dhulma baada ya kuamrishwa na afisaa mmoja wa uhamiaji
kusafiri kwenda Dar es Salaam kwani hakuwa na idhini ya mtumishi mkuu wa umaa
Francis Kimemia.
Bwana Mutunga alisema
hatishiki na kuwa hahitaji idhini kutoka kwa Kimemia kabla ya kusafiri kwenda
nje ya nchi.
Pia ameelezea wasiwasi
kuwa majaji wanatishwa kisiasa huku nchi ikiwa inaelekea katika uchaguzi mkuu.
Mutunga amesema
hatatishika kwani amekuwa mmoja wa wapiganiajai wa demokrasia Kenya na kwamba
yuko tayari kwa lolote wanalompangia.
Chini ya uongozi wa
jaji mkuu huyu, idara ya mahakama imeweza kusifiwa kwa mageuzi makubwa kwani
sasa inaonekana kuwa huru na kuwa ni vigumu kuwashawishi majaji kuegemea upande
wowote
0 Comment to "JAJI MKUU KENYA ADAI KUTISHWA KISIASA"
Post a Comment