Kinyang'anyiro, cha
uchaguzi utakaofanyika Jumatatu kinaingia mkondo wa lala salama hii leo, na
Ijumaa huku wagombea wakienda kwenye majimbo kuwaomba watu kura.
Kura za maoni
zinaonyesha ushindani mkali kati ya mgombea Uhuru Kenyatta wa Jubilee na Raila
odinga wa CORD.
Mshindani anayewafuata
ni Musalia Mudavadi wa muungano wa Amani na anashikilia nafasi ya tatu nyuma ya
wawili hao kulingana na kura za maoni.
Kwa mgombea kushinda
uchaguzi lazima apate zaidi ya asilimia hamsini na takriban asilimia 25 ya kura
katika nusu ya majimbo 47.
Miungano ambayo
inaongoza kwenye kura zamani inatumia mbinu mbali mbali kuwashawishi wapiga
kura kujitokeza siku ya kupiga kura.
Muungano wa CORD wake,
Raila Ofinga, ulisema kuwa unawataka watu 330,000 kuwaombea kura kwa wapiga
kura kote nchini.
Bwana Kenyatta amekuwa
akiwashawishi wapiga kura kupiga kura mapema kabla ya kuelekea kazini na makwao
wakati mgombea mwenza wake William Ruto,amewataka vijana kuhakikisha kuwa
marafiki zao na jamaa zao wameweza kupiga kura.
Jimbo la Rift Valley, moja
ya majimbo makubwa, ina kata 14 ikiwa na wapiga kura milioni 3,373,853. Eneo
hilo linatazamiwa kama ngome ya William Ruto.
Utafiti wa mwisho
uliofanywa kuhusu maoni ya watu kuwahusu wagombea wakuu, ulionyesha kuwa
Kenyatta angemshinda Raila asilimia 60 kwa asilimia 23.
Pande hizo mbili hata
hivyo zina matumaini ya kuibuka mshindi.
Kwa upande wake,
Muungano wa Jubilee wake Kenyatta umeelezea matumaini makubwa, ukitaka kushinda
kiwango kikubwa cha kura.
Mkoa wa kati ndio wa
pili wenye idadi kubwa zaidi ya wapiga kura na eneo hilo ni ngome ya Uhuru
Kenyatta.
Kura zote za maoni,
zinawaweka zinaonyesha kuwa Kenyatta anaweza kushinda asilimia tisini ya kura
katika eneo hilo.
0 Comment to "LALA SAMALA YA UCHAGUZI NCHINI KENYA"
Post a Comment