Awali kulikuwa na
taarifa kuwa mgombea wa Urais Uhuru Kenyatta alikuwa amesusia mdahalo huo
akidai kuwa mdahalo wa kwanza waliokuwa wanauendesha mjadala wenyewe
waliangazia sana swala la ICC na kuwafanya wagombea wengine kumlemea.
Uhuru pamoja na mgombea
mwenza William Ruto, wanakabiliwa na kosa la kuwa washukiwa wakuu wa ghasia za
baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/2008 katika mahakama ya ICC.
Duru zilisema kuwa
Uhuru alisitisha kampeini zake leo ili kuweza kujiandaa vilivyo kwa mjadala
huo.
Wagombea wengine
akiwemo waziri mkuu Raila Odinga wanajiandaa kwa mjadala huo ambao jana jioni
ulilipa kipao mbele swala la ardhi, sera za kigeni, na uchumi.
Kura za maoni
zinaonyesha kuwa asilimia tisini ya wapiga kura wanaona mjadala huu una manufaa
kwa wakenya. Asilimia themanini na tano walisema wako tayari kutazama mjadala
huo.
Asilimia robaini ya
wapiga kura waliohojiwa punde baada ya mjadala wa kwanza walisema wangempigia
kura Uhuru Kenyatta wakati asilimia 33 walisema wangempigia kura Raila
Odinga.Wawili hao ndio wagombea wakuu katika uchaguzi huu.
0 Comment to "MDAHALO WA MWISHO WA WAGOMBEA WA UCHAGUZI NCHINI KENYA ULIOFANYIKA JIONI YA JANA"
Post a Comment