Timu ya Simba ya
Dar es Salaam, jana imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa jana jioni katika Uwanja wa
Taifa.
Bao la Mtibwa
Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika dakika ya 19, baada
ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba moja wa timu hiyo, Juma
Kaseja.
Bao hilo
limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezu mtafaruku mkubwa
baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba, walikuwa wakishinikiza kutaka
kuonana na viongozi wao ili kuzungumza falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano
mkuu wa dharula.
Aidha mashabiki
hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo hadi walipotawanywa
na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha maji ya kuwasha, huku vingozi
wa timu hiyo na wachezaji wakiwa wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika
uwanjani hapo.
Hata hivyo
katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi nyekundu baada ya
kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha pili.
0 Comment to "SIMBA IMEKUBALI KICHAPO CHA BAO 1-0 DHIDI YA MTIBWA SUGAR"
Post a Comment