Wednesday, April 17, 2013

BI KIDUDE AFARIKI DUNIA




Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vinavyoaminika, Bi Kidude amefariki mjini Unguja baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa nyumbani kwake maeneo ya Rahaleo.

Pia umri mkubwa nao unasemekana kuchangia kifo chake japo hadi mauti yakimfika alikuwa hafahamu umri wake halisi.

Bi Kidude atakumbukwa sana kwa umahiri wake wa kuimba na kucheza licha ya umri mkubwa aliokuwanao ambapo aliweza kutamba na nyimbo zake kadhaa kama Ya Laiti, Muhogo wa Jang'ombe n.k.

Kutokana na umahiri wake, Bi Kidude aliweza kupata mialiko kadhaa ya kutumbuiza katika nchi kadhaa za Ulaya ikiwamo Ujerumani.

Habari za uhakika zinasema kwamba mpaka mauti yakimfika Bi Kidude alikuwa hajabahatika kupata mtoto.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

Share this

0 Comment to "BI KIDUDE AFARIKI DUNIA"

Post a Comment