Serikali ya Uganda
inasema kuwa imesitisha msako wake wa kiongozi mtoro wa waasi wa LRA Joseph
Kony, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Uganda inasema imeamua
kuchukua hatua hiyo kufuatia mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo baada ya
rais Francois Bozize kung'olewa mamlakani.
Pia imeelezea kuwa
serikali ya mpito inayoongozwa na kiongozi wa waasi imetatiza shughuli zao.
Uganda inasema kuwa
wanajeshi wake katika eneo hilo ambako waasi walichukua mamlaka siku kumi
zilizopita, watasalia katika kambi zao hadi muungano wa Afrika utakapotoa
mwongozo.
Joseph Kony anayeongoza
kundi la waasi wa LRA, anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa tuhuma
za uhalifu wa kivita.
Anaaminika kujificha na
wapiganaji wake katika misitu inayopakana na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Sudan
Kusini na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
0 Comment to "MSAKO WA KONY WASITISHWA AFRIKA YA KATI"
Post a Comment