Wafanya kazi za uokozi wamekuwa wakipata shida
kufika kwenye vijiji vya mbali milimani vilioko kusini-magharibi mwa Uchina,
baada ya tetemeko la ardhi ambalo linalijulikana kuuwa watu 200 na kujeruhi
zaidi ya 11,000.
Wanajeshi na wasamalia wakiokoa watu.
Wanajeshi 17,000
wametumwa huko kwenda kusaidia. Tetemeko hilo lilitokea Jumamosi asubuhi karibu
na mji wa Ya'an katika jimbo la Sichuan.
Waokozi wamekuwa
wakijaribu kupanda barabara nyembamba zilizozongwa na maporomoko.
Lori moja la
jeshi lilobeba wanajeshi 17 lilipinduka mlimani na kumuuwa mwanajeshi mmoja na
kujeruhi wengine saba.
Magari ya kubeba
wagonjwa yanawapeleka manusura katika kituo kwenye hospitali kuu mjini Ya'an.Majeruhi
wengi, baadhi yao wamevunjika viungo, wanatibiwa kwenye mahema yaliyowekwa nje
ya hospitali.
Tetemeko hili
lilikuwa ni dogo likilinganishwa na lile la mwaka 2008 ambalo liliuwa watu
70,000.Lakini kwa sababu ya shida za kuwafikia manusura na vitetemeko vidogo
vinavoendelea wakati wote, idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.
0 Comment to "TETEMEKO NCHINI CHINA"
Post a Comment